TOP HORIZONTAL BAR

Thursday 7 April 2016

Habari wana-Njombe kwa ujumla wetnu. Wana-Njombe ni wamoja kwa maendeleo ya  Njombe yetu. ninayo furaha kubwa kuielezea Njombe kua ni moingni mwa mikoa michache inayopata mvua nyingi na hivyo kuwa miongoni mwa mikoa inayozalisha kwa wingi zao la viazi, mahindi, miti ya kupandwa na mazao
mengine ambayo ni ya mhimu zaidi kwa ustawi na ukuaji wa uchumi wa mkoa, watu wake pamoja na nchi kwa ujumla wake.
Kinachonisiskitisha ni pale ambapo naona muamko wa jamii ya wana-njombe juu ya upandaji miti imekuwa ni kubwa hata ikafikia hatua ya kuhatarisha au kutishia usalama wa chakula katika maeneo mengi ya mkoa huu. Kinacholeta mashaka ni pale ambapo wakazi wengi wa mkoa huu wameamua kujikita zaidi na kilimo cha miti hata kusahau kilimo cha mazao ya chakula ambayo yangeweza kuwapelekea uwepo wa chakula cha kutosha. Kama ukifuatilia kwa kina zaidi tabia za wakazi wengi wa maeneo hay mengi kwa sasa wameamua kuacha uzalishaji wa nafaka na kujikita zaidi na upandji miti wakati wa msimu wa kupatnda au kupalilia mimea shambani. Kinachohudhunisha zaidi ni pale ambapo watu wengine wameamua kuanza kutumia mashamba yao ya kulimia chakula au nafaka kuanza kutumiwa kama mashamba ya upandaji wa miti na hivyo kutishia usalama wa chakula kwa muda wa miaka michache ijayo. kwa huyo hatua za makusudi zinahitajika kuchukuliwa ili kunusulu  balaa kubwa linaloweza kujitokeza hapo baadae.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts