TOP HORIZONTAL BAR

Thursday 4 August 2016

brightfuture

1 comment:

  1. Ushauri wangu wanadada wanaotaka haki sawa.
    Katika maisha yetu ya kila siku kuna vitu vidogo ambavyo watu huwa hatuvizingatii, lakini vina mchaango mkubwa sana kushawishi mamlaka ya mtu katika sehemu anayoishi. kwa kawaida mtu huwa anahaki ya kudai haki yake katika mazingira yoyote ikiwa mtu huyo anahisa ama anasabau ya msing inayompa ushiriki wake hiyo katika hicho anachotaka kudai.
    Kunamtaalam mmoja wa utafiti wa mambo ya haki za binadamu anasem kuwa mtu hawezi kuwa na haki na hawez kuhesabiwa haki ikiwa hana mchango wowote katika hiyo haki anayoitaka. Mtaalamu huyo anatumia mfano wa mkulima na mtaalam wa kilimo kulielzea hili akisema kuwa; kama mkulima hata changia kiasi chochote hata kama ni kiasi kidogo tu, basi mkulima huyo hawezi kuwa na hakikudai ama kuuliza ubora wowote katika huduma atakazokuwa anapewa. Hivyo mkaulima huyo husubili maagizo kutoka kwa ataalam au wawezeshaji wengine ili atekeleze maagizo hayo. mfano huu ni sawia kabisa na maisha wanayoyachagua akina dada wengi kuyaishi. nasema wwanyachagua kwa sababu ni uamuzi wa akina dada wenyewe kuishi maisha ya mtu (mwanamme). Utashangaa sana kuona akina dada wengi wakifikiria kuolewa na wanaume wenye hela, mishahara mizuri na wanaomiliki mali nyingi wakidhani kwa kufanya hivyo ndio wataishi maisha mazuri na kwa furaha. Ama kweli uwezo wa wadada wengi kufikiri na kuamua uliathiriwa na mfumo dume kama wasemavyo wao.Katika uhalisia wa maisha huwezi kuwa na haki yoyote katika kitu ambacho wewe huna mchango wowote kwenye uwepo wa hicho kitu. Kwa namna ya haraka mimi binafisi hupenda kulinganisha wanawake wa aina hii na wafanyakazi wa ndani yaani "house girls" kwa sababu kama ilivyo kwa house girl,huja hana mali yoyote akitegemea kutumia mali za bosi wake na hivyo hupangiwa na kuamuliwa katika kila kitu. Maana hii ni sawa kabisa na mwanamke anayeishi na mwanamme akiwa hana mchango wowote ambapo naye huishia kupangiwa na kuamuliwa na mumewe katika kila kitu. Na hapo ndipo utakaposikia eti kuna unyanyasaji wa kijinsia.
    Kama mimi ningekuwa mshauri wa jamii ningeshauri akina dada kabla ya kuolewa wasijiulize mtu anayeolewa naye anamiliki mali gani na anapesa kiasi gani, baadala yake wajiulize huyo mtu anamchango gani ama watasaidiana vipi kufikia malengo yenu na sio kuangalia anamiliki kitu gani wakati hata hujui alivipata vipi. Najiuliza mbona wanaume wengi hawachagui wanawake wenye hela badala yake wanafikiria kumpata mke mchapa kazi na anayewaheshimu na kujiheshimu.Nafikiri labda wanawake wengi wao wanafikiria kutegemea mtu mwingine ili wafanikiwe ndo maana mara nyingi huhitaji wanaume wenye hela au mali nyingi katika maisha yao.Na kama ndivyo, basi vita zidi ya mfumo dume ni ndoto za mchana kufanikiwa kwake. Endelea kufuatilia mjadala huu utaendelea hivi karibuni.....................

    ReplyDelete

Popular Posts